The House of Favourite Newspapers

Mvua Yaua 13 Morogoro, Wakiwemo wanafunzi 9

 

MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro zimesababisha vifo vya watu 13 miongoni mwao ni watoto tisa wenye miaka kati ya 11 na 15.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio la kwanza ni la watoto watano waliofariki baada ya kuzama katia Mto Mvuha uliopo kata Kibogwa

Watoto hao ni Neema Rajabu (10), Latifa Khalid (9), Munila Khalid (11), Omary Khalid (14)  na Zanisha Adam (9) ambaye mwili wake bado haujapatikana na shughuli ya kumtafuta inaendelea.

Mutafungwa alibainisha kuwa Said Rajabu (11) mwanafunzi wa darasa la tatu aliyekuwa na wenzie waliokufa alinusurika na kujeruhiwa baada ya kuona maji yakizidi ambapo alikimbia na baadaye alianguka na anaendelea na matibabu katika zahanati ya Kibogwa.

Wengine waliokufa ni wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Kibwaya Tarafa ya Mkuyuni, Rajabu Issa (11) na Shabani Msimbe (15), baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji walipokuwa wakiogelea. Wanafunzi wengine wawili waliokufa maji ni Karim Athuman (13) na Hussein Hassan (14) wa Shule ya Msingi Ulundo waliozidiwa na maji wakiwa wanaogelea kwenye Mto Ngerengere.

Comments are closed.