The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo Kupanda Ulingoni Februari Hii

0


Bondia anaefanya vizuri sasa hivi Tanzania Hassan Mwakinyo anatarajia kurejea ulingoni Februari 25 mwaka huu katika pambano lililopewa jina ‘MABINGWA WA ULINGO’ huku safari hii ikiwa ni kwa msimu wa pili na pambano litapigwa ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Katika pambano hilo ambalo si la ubingwa Mwakinyo anatarajiwa kucheza dhidi ya bondia namba nne kwa ubora nchini Venezuela, Ivan Matute mwenye rekodi nzuri ya kucheza jumla ya mapambano 34 ya ngumi za kulipwa huku akishinda mapambano 30 na kupoteza mapambano 4 huku mawili akipigwa kwa KO.

Siku hiyo kutakuwa na pambano kuu lingine ambapo Tony Rashidi atarudiana na bondia kutoka Afrika kusini Bongani Mahlangu, na itakumbukwa Bongani alimchakaza Tony Rashidi kwa KO hapahapa Tanzania mwezi Septemba mwaka jana.

Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha tembelea Msasa Online kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24.

Leave A Reply