The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo Kuwania Mkanda Wa WBO Agosti Mwaka Huu

0
Hassan Mwakinyo

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni kuwania Mkanda wa Dunia wa WBO chini ya Kampuni ya Promosheni ya Ngumi za Kulipwa ya PAF, Agosti mwaka huu.

Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo, alisema kwa sasa amejipanga kuhakikisha anakata kiu ya Watanzania katika mchezo wa ngumi za kulipwa kwa kucheza pambano la kuwania mkanda huo ambao hajauwahi kuchezwa nchini.

“Natarajia kupanda ulingoni mwezi ujao katika pambano kubwa la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBO.

“Muda mrefu nilikuwa natamani nipate pambano kama hili, lakini nilikuwa bado sina vigezo, sasa nashukuru nimevipata na utakuwa wakati mzuru sana kwangu kupata pambano hili. Ningefurahi pia kwa mabondia wa Tanzania na wao wangepata nafasi kama hii tena wakipigana hapahapa nchini lakini bado vigezo hawana,” alisema Mwakinyo na kuongeza.

“Ukimya wangu haukuwa wa bure, nitakidhi kiu ya mashabiki wangu ambao hawajaniona muda mrefu ulingoni. Nitawastarehesha na kuwaburudisha mashabiki wangu. Nimejiandaa na bado najiandaa vyema mpaka sasa kwa pambano hilo.

“Kwa Tanzania, boksa yeyote anayetaka kupigana na mimi kwanza agombee mkanda huu ninaokwenda kuupigania. Lakini pia hata mabondia wakubwa huwa wanacheza sparling, hivyo kama kuna bondia anataka hivyo aje Masaki tupigane.”

STORI NA IBRAHIM MUSSA

#EXCLUSIVE: MWAKINYO AMLIPUA TWAHA KIDUKU – “SIWEZI KUPIGANA KAMA HATUENDANI”…

Leave A Reply