Mwakyembe: Tunahitaji Ushindi Katika Soka Dhidi ya Yeyote
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Harison Mwakyembe, usiku wa kuamkia leo alipata fursa ya kula chakula cha pamoja na wachezaji wa kikosi cha Taifa Taifa Stars ndani ya Sisicape Hotel iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambao wanajitayarisha katika mashindano ya Kagame Cup yatakayofanyika mwezi ujao (Seemba) mwaka huu..
Mwakyembe alitumia muda huo kuwaaga wachezaji hao ambapo leo asubuhi wamekwenda nchini Kenya kushiriki katika michuano ya Kagame Cup.
Akiwaaga. amewataka wayatumie mashindano hayo kuiletea Tanzania heshima ya ubingwa kwani wana kila sababu ya kufanya hivyo kwani Serikali ipo nao huku akiwata wahakikishe wanashinda kila mchezo ulio mbele yao.
“Ninatambua uwezo wenu ni mkubwa kama mwalimu wemu alivyosema, hakikisheni mnamtandika kila atakayekuja mbele yenu, mimi nitakuja mchezo wa pili mkishinda.
“Makipa watatu nawajua wako poa lakini hata ‘straikaz’ wako safi na beki nawajua wachache lakini wapo safi
Hivyo hadi hapo sina wasiwasi na mchezaji yeyote kati yenu zaidi mcheze mkijua Watanzania wapo nyuma yenu na wanahitaji ushindi,” alisema Mwakyembe
Kikosi hicho jana kimeongeza wachezaji watatu wapya ambao ni Yahaya Zaydi (Azam) nafasi ya straika,
Amani Kaita (Nakuru All Stars Kenya) ambaye anacheza nafasi ya kiungo na Ramadhani Kabwili kipa waklabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
(HABARI/PICHA; MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS)