The House of Favourite Newspapers

Mwalimu aeleza ziro ya hesabu ya Samatta

0

IMG_4266
Mwalimu akihojiwa na mwandishi wa habari(hayupo pichani).

Na Ibrahim Mussa
FURAHA ya Watanzania bado inaendelea kushika kasi kutokana na mafanikio ya ushindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ndani, iliyotwaliwa na Mtanzania, Mbwana Samatta.

Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutwaa tuzo hiyo.

hampioni limefanikiwa kufika katika shule aliyosoma mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, inayofahamika kwa jina la Thaqalaini iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam na kuzungumza na mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuru Mhina, ambaye amezungumza mengi kuhusu staa huyo.

Unamzungumziaje Samatta kama mwanafunzi wako?
“Kweli Samatta alianza hapa kidato cha kwanza mwaka 2005 na kumaliza kidato cha nne mwaka 2008, masomo yake aliyokuwa anayapenda ni ya Sanaa ‘Arts’ kwa sababu alikuwa hajui kabisa hesabati.

IMG_4285

Mwalimu akiwa kwenye mazingira ya shule.

“Kuhusu suala la nidhamu, Samatta hakuwa na tatizo hata kidogo, lakini tulikuwa tunakorofishana sana katika suala la utoro kwa sababu kuna wakati tulikuwa hatujui kwa nini alikuwa hafiki shuleni, kuna wakati ilibidi tuwaite wazazi wake ili kuongea nao na kwa bahati nzuri tuliweza kulimaliza tatizo hilo.

“Lakini nakumbuka wakati huo sikuwa mkuu wa shule, hivyo kipindi chake alikuwa akisumbuana na mwalimu wake mmoja wa michezo anaitwa Juma Posi ambaye kwa sasa hayupo.

“Hakuwahi kupata adhabu yoyote, ila adhabu alizoweza kuzipata ni zile ambazo zilikuwa zinahusu wanafunzi wa darasa zima, lakini kwa peke yake hakuwahi kupata maana alikuwa mpole mno na hata makazi yake darasani yalikuwa nyuma kabisa na mwalimu alikuwa anaweza kuingia na asijue kama yupo au hayupo.

IMG_4263

Shule aliyosoma Mbwana Samata.

Vipi katika timu ya shule alikuwa na msaada?
“Samatta alikuwa na msaada mkubwa katika timu ya shule kwa sababu ndiyo kitu alichokuwa akipenda na hata wanafunzi wenzake walikuwa wakimpenda kwa sababu alikuwa anajua sana soka.

“Ulikuwa ukikutana naye nje ya uwanja huwezi kujua kama anaweza kucheza soka kwa kiwango hicho.
“Lakini nakumbuka kuna wakati alishawahi kutufanyia uhuni katika mashindano ya Umiseta wakati tulipokuwa tunacheza na moja kati ya wapinzani wetu, timu ya Shule ya Al-Furqan.

IMG_4291“Tulikuwa tunamtegemea sana lakini siku hiyo hakutokea uwanjani mpaka dakika 15 kabla mchezo haujamalizika ndiyo alifika, na mechi hiyo tulifungwa.

Vipi aliweza kufanya mtihani wake wa mwisho?
“Kiukweli mtihani wa mwisho wa kidato cha nne, Samatta aliweza kufanya yote ila kwa bahati mbaya hakuweza kufaulu kwa maana alipata ziro kabisa likiwemo somo la hesabu.

“Lakini kuna kitu tumejifunza kupitia Samatta hasa kuhusu michezo kwa sababu ugomvi wetu ulikuwa unatokana na suala la taaluma maana walimu na wazazi siku zote tumekuwa tukielewa kuwa elimu ndiyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu ila kwake imekuwa tofauti.

IMG_4286“Angalia leo hii Samatta huyu ambaye hakuwa mzuri kitaaluma lakini ameweza kuwa mtu mkubwa na mwenye utajiri katika nchi hii kuliko sisi walimu wake.

“Kutokana na hili basi tumeamua kuhakikisha shule inaanzisha kitengo cha masomo maalum ya michezo ikiwemo mambo ya uchoraji na soka ili tuweze kutoa fursa kwa wanafunzi wetu waweze kutimiza ndoto zao kama ilivyokuwa kwa mwenzao ambaye kwa sasa hata shule imekuwa ikisifiwa kupitia yeye.

IMG_4222

Mbwana Samatta enzi za utoto.

Mna mpango gani na Samatta?
“Tuna mpango wa kumualika aje hapa shuleni kabla hajaondoka ili tuweze kumpa zawadi tutakayoweza kumuandalia pamoja na kutoa hamasa kwa wanafunzi wetu ili wapende michezo kwa sababu hakuna anayejua kesho itakuwaje.”
Mwisho

Leave A Reply