The House of Favourite Newspapers

Mwalimu Aliyemfundisha Diamond Kiingereza Afunguka Jinsi Ilivyo Rahisi Kujifunza Lugha Hiyo

0

Mwalimu aliyepata umaarufu kwa kumfundisha staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz Kiingereza, Allen Ngonyani almaarufu Teacher Allen amefunguka kuwa ni rahisi kwa mazingira ya Tanzania mtu kujifunza Kiingereza kwa muda mfupi na kuwa na uwezo wa kuzungumza vizuri.

Amesema kwa kawaida, mwanafunzi akiwa mwepesi, ndani ya miezi tisa pekee atakuwa na uwezo wa kuzungumza vizuri kabisa hata kama awali alikuwa hajui chochote.

Teacher Allen ndiye aliyemfundisha Diamond Kiingereza na kumfanya awe na uwezo wa kuzungumza vizuri lugha hiyo tofauti kabisa na ilivyokuwa awali ambapo pia amewasaidia watu wengine wengi kuijua lugha hiyo.

Video kamili ipo Youtube, Global TV.

Leave A Reply