The House of Favourite Newspapers

Mwambusi aipa ushindi Simba

0

Juma-Mwambusi-coach-Yanga

Juma Mwambusi.

Sweetbert Lukonge,
Dar es Salaam
TIMU ya Simba, Jumamosi hii inashuka uwanjani kupambana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi iliyopo baina ya timu hizo mbili kila zinapokutana kwenye uwanja huo.

Hata hivyo, kiungo mshambuliaji wa Simba, Mwinyi Kazimoto, ameliambia gazeti hili kuwa, safari hii lazima Mbeya City wakae katika mechi hiyo kutokana na akili zao kwa sasa kutawaliwa na simanzi kubwa ya kuondokewa na kocha wao kipenzi, Juma Mwambusi.

Alisema kwa hali hiyo ni kama Mwambusi amewapatia ushindi Simba katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Jiji la Mbeya.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu kwa ajili ya mechi hiyo na safari hii lazima tuibuke na ushindi kwa sababu jamaa hivi sasa hawapo vizuri kisaikolojia baada ya Mwambusi kuondoka, hakika tutahakikisha tunaitumia vizuri nafasi hiyo,” alisema Kazimoto.

Mwambusi kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Yanga, kazi ambayo ameianza juzi Jumatatu baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu akichukua mikoba ya Charles Mkwasa ambaye hivi karibuni amepewa majukumu ya kuifundisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa muda wa miaka miwili na nusu.

Leave A Reply