The House of Favourite Newspapers

Kisa penalti, Ngoma apewa adhabu Yanga SC

0

Ngoma-2

Mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Wilbert Molandi,

Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, juzi Jumatatu alijikuta akipewa adhabu ya kupiga pushapu na kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm baada ya kukosa penalti.

Mzimbabwe huyo alipewa adhabu kwenye mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Ngoma alijikuta akipewa adhabu hiyo pamoja na wachezaji wenzake waliokuwa naye timu moja, baada ya kukosa penalti.

Wachezaji wengine waliopewa adhabu hiyo ya kupiga pushapu 10, iliyotolewa na kocha huyo ni Vincent Bossou, Andrey Coutinho, Malimi Busungu, Said Makapu, Mbuyu Twite na Simon Matheo.

Timu hizo zilipiga penalti mara baada ya programu za kocha huyo kumalizika na kuzitaka timu hizo mbili zilizocheza mechi, kupiga penalti kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Azam.

Kati ya wachezaji hao waliopiga penalti, Ngoma pekee ndiye aliyekosa wakati wenzake wote wakipiga kwa ufanisi mkubwa wa kumchambua kipa Mudathiri Khamisi, ikiwemo ile ya Coutinho.

Baada ya kukosa penalti hiyo ambayo ilikuwa ya mwisho kwa timu yake, kocha wa timu hiyo aliwafuata wachezaji hao akiwataka kupiga pushapu hizo huku akiwasimamia.

Leave A Reply