The House of Favourite Newspapers

Mwana FA Ashindwa Kujizuia Kwa Lady Jaydee

0
Lady Jaydee.

RAPA Mkongwe anayetamba na ngoma ya Dume Suruali, Mwana FA  ameshindwa kuvumilia na kuvunja ukimya kwa kuonyesha sapoti kwenye video ya ngoma mpya  ya Mkongwe Lady Jaydee ‘I miss you’ ikiwa ni miaka takribani minne tangu fukuto la bifu lao.

Kupitia kwenye ukurasa wa Instagram Mwana FA ameweka video ya wimbo huo ambayo imeachiwa leo huku akiwataka watu kwenda kuitazama video hiyo kwenye mtandao wa You tube.

Mwana FA ameandika kwa lugha ya Kingereza akimaanisha  “Video ya wimbo mpya wa Lady Jaydee  ” I Miss You”  hatimaye umetoka  furahia  karibu”...na Lady Jaydee akashukuru kwa ufupi kwa kuandika kwa lugha ya kingereza akimaanisha  “Baraka nyingi”

Hata hivyo jambo hilo limeonekana kuwafurahisha mashabiki wengi wakiwepo wasanii wenzao ambao pia ni watu wao wa karibu kwa kuandika jumbe mbalimbali.

Mwanamuziki Ambwe Yessaya  ameandika   “Manka weee  Lady Jaydee umetisha sana, nangojea siku yetu ya nyama ndio nikupe vocha…Mwana FA

Mbunge wa Mikumi na Mkongwe wa Rap nchini Professor Jay naye ameandika “Thats True LOVE MISS U TOO Guy” @mwanafa @jidejaydee @aytanzania

Mbali na hao mashabiki wengi nao wamefurahishwa kwa kitendo hicho kupitia ujumbe huo na kuwataka wawili hao waweze kufanya tena kazi kwa pomoja.

Wawili hao inadaiwa kuwa vuguvugu la bifu lao lilianza mnamo 2013 na Mwanamuziki Lady Jaydee amekuwa akinukuliwa kwamba hakupendezwa na jinsi rafiki yake huyo (Mwana FA) alivyotumiwa na maadui zake kutaka kumuharibia tamasha lake.

Lady Jaydee kwa sasa ana Video Mpya inayokwenda kwa jina la ‘I miss you’ itazame hapa chini.

Leave A Reply