The House of Favourite Newspapers

Mwana: Maprodyuza wapenda ngono wananiboa

0

Mwanaheri-A-534Stori: IMELDA MTEMA

Msanii anayekuja kwa kasi katika  tasnia ya filamu Bongo, Mwanaheri Ahmad, amefunguka kuwa wasanii wengi wanazidi kudidimiza vipaji vyao kutokana na tabia za maprodyuza ambao wanapenda ngono.

Akizungumza na gazeti hili Mwanaheri, alisema msanii anaweza kuwa ana kipaji kabisa lakini anaweza kuachwa na prodyuza kwa sababu tu amemkatalia anachotaka hivyo akampa mtu mwingine ambaye hana uwezo wa kucheza filamu hiyo.

“Jamani tabia tu ya maprodyuza ndiyo inanipa changamoto kubwa sana katika kazi yangu maana watu wenye vipaji wanaachwa kabisa wanachukuliwa watu wengine,” alisema Mwanaheri.

 

Leave A Reply