The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Agongwa na Basi la Al Saedy, Afariki Dunia

0

MWANAFUNZI Nurdin Ally (6) amefariki dunia baada ya kugongwa na basi kampuni ya Al Saedy lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu ameiambia Habarileo kwamba basi hilo lenye namba za usajili T 296 CYT lilimgonga mtoto huyo ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mkundi. Mtoto huyo alikuwa akitoka shule.

Amethibitisha kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi Lung’wawa barabara ya Morogoro — Dodoma majira ya mchana. “Mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro hata hivyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu,” alieleza.

Abiria waliokuwa kwenye basi hilo walitoka salama na baadae kuruhusiwa kuendelea na safari. Hata hiyo, Musilimu alisema dreva wa basi hilo alikimbia na kulitelekeza na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.
Imeandaliwa na Agnes Haule.

MWANAFUNZI Nurdin Ally (6) amefariki dunia baada ya kugongwa na basi kampuni ya Al Saedy lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amethibitisha kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi Lung’wawa barabara ya Morogoro – Dodoma majira ya mchana.

Kamanda Musilimu amesema kwamba basi hilo lenye namba za usajili T 296 CYT lilimgonga mtoto huyo ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mkundi ambaye alikuwa akitoka shule.

“Mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro hata hivyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu,” alieleza.

Abiria waliokuwa kwenye basi hilo walitoka salama na baadae kuruhusiwa kuendelea na safari. Hata hiyo, Musilimu alisema dreva wa basi hilo alikimbia na kulitelekeza basi hilo ambapo jeshi la polisi linaendelea kumsaka.

Leave A Reply