The House of Favourite Newspapers

Baba wa Askari Aliyejinyonga Mahabusu “Hakuna Picha Inayoonyesha Amejinyonga”

0

Gaitan Mahembe, ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi anayedaiwa kujinyonga, Greyson Mahembe akiwa mahabusu mkoani Mtwara amesema alipewa taarifa kuwa mwanae ameshikiliwa kwenye mahabusu ya Polisi, na Januari 22, 2022 nilipigiwa simu kuwa bahati mbaya mwanae amejinyonga, jambo ambalo lilimstua.

 

Gatian na askari wenzake sita walikamatwa kwa tuhuma za mauaji ya kijana Mussa Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7 ambapo baadae ilielezwa kuwa amejinonga kwa kutumia tambala la deki hadi kufa.

 

“Polisi walifanya mambo haraka, wakaleta mwili hadi kwangu Segerea haraka walipofika wakawa wanasema shusha hapa, tukakataa nusura tupigane, tukawaambia mwili huu ukahifadhiwe kisha tuje hapa tuzungumze.

 

“Tuliwaambia askari waliouleta mwili, safari yetu ni ya Iringa lakini hatuwezi kuupokea hadi mtueleze, mwanangu ni afisa wa jeshi alitakiwa asindikizwe kijeshi na azikwe kijeshi kwanini halikufanyika hilo.

 

“Kama mwanangu alijinyonga wangeitwa ndugu upande wetu wakathibitishe au tungeoneshwa picha hata za kutoka jeshi la polisi zikionesha amejinyonga, au picha zozote kwenye vyombo vya habari. Hakuna hilo.

“Ndugu yetu aliitwa wakati marehemu alishapelekwa hospitali ya Ligula na akaoneshwa michubuko akielezwa ni ya kamba, kisha akaambiwa ni ya tambara la deki, hivi mahabusu ya jeshi kuna tambara la deki?” 

“Mimi na familia yangu hatujaridhishwa, tunamuomba IGP alifafanue hili na ukweli uwekwe wazi. Hatuna kipato, hivyo tunaomba tupate mwanasheria wa kujitolea au wa serikali akatusaidia katika hili tutashukuru”

“Hakuna picha inayoonesha marehemu alijinyonga au ananing’inia, ukweli wake ndio uliomponza, marehemu alisema kwanini nihangaishwe wakati mimi nilitumwa? wakubwa wenyewe wapo, mimi nilikuwa ni mtekelezaji” amesema Mzee Gaitan Mahembe.

Leave A Reply