The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Apigwa Risasi na Kuzikwa Katika chuo Kikuu cha Sudan

0

Mwanafunzi mmoja ameuawa katika Chuo Kikuu cha Khartoum baada ya kupigwa risasi huku kukiwa na mapigano makali katika mji mkuu wa Sudan.

Mwili huo ulizikwa chuoni baada ya kushindwa kupita kwa usalama kutoka kwenye eneo hilo lililokuwa halijalindwa.

Sudan imekumbwa na ghasia tangu mvutano ulipotanda kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo maarufu wa RSF.

Baadhi ya wanafunzi bado wamekwama katika eneo hilo.

“Tulimzika rafiki yetu baada ya kupata ruhusa kutoka kwa familia yake na chuo kikuu. Tulikuwa tunaenda kupata chakula kwa ajili wanafunzi wengine,” mwanafunzi wa sheria Mosaab Sharif, ambaye anajihifadhi katika jengo karibu na chuo kikuu, aliiambia BBC.

“Tulikuwa watatu, lakini yeye alipigwa kifuani. Hatukuweza hata kumsaidia. Wakati tunamzika mwenzetu mmoja alipigwa risasi mkononi.”

Jeshi na kundi la wapiganaji laRapid Support Forces (RSF) wanadai kudhibiti maeneo muhimu mjini Khartoum, ambapo wakazi wamekuwa wakijikinga na milipuko na milio ya risasi.

“Watekaji nyara wamekuwa wakilenga mtu yeyote aliye na taa za kuangaza. Ndiyo maana hakuna anayetembea akiwa amevalia nguo nyeupe ili kuwa salama zaidi,” alisema Bw Sharif.

“Tunaziogopa pande zote mbili, jeshi na RSF, ikiwa watapiga risasi kuelekea kwetu.” Mwanafunzi huyo wa sheria pia aliongeza kuwa wanafunzi wengine walikuwa wamelala katika msikiti wa karibu, wakati ambao ganda la risasi liilipiga jengo hilo na kujeruhi watu wawili.

“Tupo katikati ya mapigano makali. Kuna mashambulio ya risasi karibu yetu ambayo yanapiga nyumba.

“Wanafunzi wamekuwa hapa kwa siku tatu bila chakula wala vinywaji. Hali yao ni mbaya sana,” Bw Sharif alieleza kwenye video iliyowekwa mtandaoni, huku milio ya risasi ikisikika kwa nyuma.

Leave A Reply