The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Chuo Kikuu Afariki Dunia Kwa Kuchomwa Visu

MWANAFUNZI wa Stashahada ya Maabara katika Chuo Kikuu cha Kampala, Tawi la Tanzania (KIU), Anifa Mgaya, amefariki dunia juzi Jumapili usiku baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.

 

Anifa alikutwa na umauti majira ya saa 2 usiku jirani na geti la kuingia katika chuo hicho kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es Dar es Salaam alichokuwa akisoma.

 

Taarifa zinaeleza baada ya kushambuliwa, wanafunzi wenzake walijitokeza ili kumpatia msaada kwa kumkimbiza hospitali lakini hadi wanafika alikuwa tayari umauti umemfika.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha vijana waliohusika katika tukio hilo wanasemekana kuwa ni vibaka.

Comments are closed.