The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Kidato cha Nne Ajiua kwa Bastola ya Profesa

JASMIN NGOYE (18) mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Lupanga iliyopo manispaa ya Morogoro, amekutwa amekufa baada ya kujipiga risasi ya kichwa huku chanzo cha kifo hicho kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.

 

Tukio hilo limetokea Jumanne Februari 19, 2019 eneo la Kola B Mtaa wa Bogwa ambapo mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ukiwa na bastola aina ya Bereta pembeni, magazini moja na ganda la risasi.

 

Akizungumzia tukio hilo jana Alhamisi Februari 21, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alisema muda mfupi baada ya tukio hilo, shemeji wa binti huyo, Profesa Hamisi Mahigi, alijitokeza na kueleza kuwa bastola hiyo ni yake na anaimiliki kihalali.

 

Kamanda huyo amesema binti huyo aliyeacha ujumbe aliouandika katika kitabu chake cha kumbukumbu kabla ya kujipiga risasi, alimkabidhi rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja, Imelda Milanzi.

 

Katika kitabu hicho mwandishi huyo ameandika; “Ni mtoto asiye na wazazi wake na asiyejua kazaliwa wapi? Mtoto huyu anatamani kukiona kifo chake wakati wowote, mtu yeyote atakayesoma dayari (diary) hii ndiye atakayeandika siku ya kifo chake.”

 

Mutafungwa alisema profesa huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

INAHUZUNISHA ! Mtoto Hamisi AWALIZA WASANII

Comments are closed.