The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi UDSM Afariki kwa Kujirusha Ghrofani Baada ya Kuiba

0

MWANAFUNZI mmoja aitwaye Manawa Samson Horera (22) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Shahada ya kwanza ya Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya pili.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro wakati akitolea ufafanuzi wa tukio hilo la aina yake na kusema tukio hilo lilitokea Januari 11, 2022 katika Hosteli za Magufuli, hapo UDSM.

 

“Mwanafunzi huyo aliingia kwenye chumba cha Mwanafunzi mwenzake aitwaye Hamza Abdulhaman na kuiba laptop aina ya HP ambapo Hamza na wanafunzi wengine walimuona, na alipobaini ameonekana na wanafunzi wenzake aliamua kuruka kupitia dirishani.

 

“Jeshi la Polisi linawataka wanafunzi kuacha kujihusisha na uhalifu kwani maeneo hayo ya hosteli yamekuwa na malalamiko ya wanafunzi laptops zao kuibiwa na watu wanaodhaniwa ni wanafunzi wenzao suala ambalo linaweza kukatisha masomo yao ikibainika ni wahalifu,” amesema Kamanda Muliro.

Leave A Reply