The House of Favourite Newspapers

Denis Nkane Yamemkuta Yanga, Nje Mwezi

0

KIUNGO Mshambuliaji waYanga, Denis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana
na kusumbuliwa na
Kinena.


Nkane alisajiliwa na
Yanga kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Biashara United, huku kwa sasa akiwa
amecheza mechi mbili
za michuano ya Mapinduzi.

 

Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya KMKM kwenye Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza na
Championi Jumatano, Daktari waYanga, Youssef Mohammed, alisema kuwa: “Kwa sasa kuna jumla ya wachezaji wanne ambao ni majeruhi kwenye kikosi.

 

“WapoYacouba Sogne, Kibwana Shomari,Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao wanaenda Tunisia kwa ajili ya
kupatiwa matibabu
na Denis Nkane.


“Denis alipata
majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ambapo kwa sasa anasumbuliwa na Kinena, tatizo ambalo litamuweka nje kwa muda wa mwezi mmoja.”

 

STORI NA LEEN ESSAU, Dar es Salaam

AZAM FC WAMEPANIA KUWAFUNGA na SIMBA, WAPIGA TIZI la KUFA MTU, FAINALI KESHO ni YAMOTO..

Leave A Reply