The House of Favourite Newspapers

Mwanafyale Apigwa KO, Kabongo, Migwede Wafanya Maajabu (Picha +Video)

0

 

Bondia Joseph Mchapeni (kulia) akimpa makonde ya nguvu Danny Mwanafyale katika pambano la Face Off ya Twaha Kiduku na Dullah Mbabe iliofanyika usiku wa kuamkia jana katika Ukumbi wa F2 Florida uliopo Msamvu mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo Agosti 15, 2021.

 

BONDIA Danny Mwanafyale usiku wa kuamkia leo Agosti 15, 2021 ameshindwa kuonyesha uwezo wake mbele Joseph Mchapeni baada ya kukubali kipigo cha KO ya raundi ya kwanza iliompelekea kuvuja damu nyingi puani.

 

Mwanafyale amepokea kipigo hicho katika pambano la Face Off ya Twaha Kiduku na Dullah Mbabe iliofanyika usiku wa kuamkia jana katika Ukumbi wa F2 Florida uliopo Msamvu mkoani Morogoro.

 

Mwanafyale na Mchapeni ambao wametrendi katika mitandao ya kijamii na kupelekea kuwa ugomzo lakini kabla ya Mwanafyale kupokea kipigo hicho kizito.

 

Lakini Kanda Kabongo amefanikiwa kumchapa kwa KO ya raundi pili Mohamed Jailani ambayo ilipelekea kulala mwenyewe kabla ya kuja kuokolewa kutokana na hali yake kuwa mbaya.

 

Pia bondia Ramadhani Migwede amefanikiwa kumbonda Mwinyi Mzengela kwa pointi wakati Grace Mwakamale akimchapa kwa pointi Asha Ngedere huku Mwanne Haji akimshinda Mwajuma Ramadhani.

 

Wengine walioshinda ni Juma Misumari amemchapa kwa kwa KO ya raundi pili Babuu Luda wakati Karim Mandonga akimpiga Omari Athumani kwa pointi sawa na Ally Mwerangi akimchapa kwa pointi Twalib Tuwa.

Wakati huohuo, bondia Dullah Mbabe ameshindwa kutokea kwenye tukio la Face Off  licha ya Twaha Kiduku kumtaka ajitokeze hadharani kabla ya pambano lao ambalo linatarajia kupigwa Agosti 20, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.

Na Ibrahim Mussa, Morogoro

DULLA MBABE vs TWAHA KIDUKU – FACEOFF, KUELEKEA PAMBANO LAO JUMAMOSI..

Leave A Reply