The House of Favourite Newspapers

Mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati Kuzikwa Leo

Waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara

Ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara, mchana wa leo.

Marehemu Sagati alifariki dunia pamoja na watu wengine wawili katika  ajali wilayani Geita.

Kiongozi wa dini akiongoza ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema ajali hiyo ilitokea  Jumatatu Septemba 30, 2018 wakati dereva wa gari lenye namba   STK 9565 aina ya Toyota Land Cruiser V8, alipomkwepa mpita njia, Happiness James (7), aliyekatiza barabarani ghafla  wilayani Chato, Mkoa wa Geita.

Alisema kutokana na ajali hiyo, watumishi wa wizara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Ludovick Nuhiye, Mchumi Nickson Matembo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Yusuph Mbwalwa na dereva, Lucas  wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita wakipatiwa matibabu.

Kamanda Mwabulambo  alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Minkoto, Kijiji cha Kalembela wilayani Chato mkoani Geita. “Gari hilo lilikuwa likitokea Mkoa wa Kagera kwenda Mwanza na  binti huyo   alinusurika kugongwa baada ya dereva kufanya jitihada za kumkwepa.

“Dereva alilazimika kupeleka gari upande wa kulia ambako pia alikutana na kumgonga na mpitanjia,   Semeni Kibiriti,  ambaye alifariki dunia hapo  hapo.

Comments are closed.