The House of Favourite Newspapers

Mwanaharakati aliyeko kifungoni Narges Mohammadi ashinda tuzo ya Amani ya Nobeli

0

Anapigania wanawake dhidi ya ubaguzi wa kimfumo na ukandamizaji, alisema Berit Reiss-Andersen, mwenyekiti wa Kamati ya Nobel ya Norway ambaye alitangaza tuzo hiyo huko Oslo.

Mwanaharakati aliyeko kifungoni Narges Mohammadi alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel leo Ijumaa kwa kupambana kwake na ukandamizaji wa wanawake nchini Iran.

Anapigania wanawake dhidi ya ubaguzi wa kimfumo na ukandamizaji, alisema Berit Reiss-Andersen, mwenyekiti wa Kamati ya Nobel ya Norway ambaye alitangaza tuzo hiyo huko Oslo.

Mamlaka ilimkamata Mohammadi mwezi Novemba baada ya kuhudhuria ukumbusho wa muathirika wa maandamano ya ghasia ya mwaka 2019. Mohammadi ana historia ndefu ya kifungo, hukumu kali na pia wito wa kimataifa umetolewa kwa ajili ya mapitio ya kesi yake.

Kabla ya kufungwa jela, Mohammadi alikuwa makamu wa rais wa Kituo kilichopigwa marufuku cha Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Iran. Mohammadi amekuwa karibu na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya Iran Shirin Ebadi, ambaye alianzisha kituo hicho.

MAPYA YAIBUKA DADA ALIYEDAI KUNYANG’ANYWA MTOTO na BOSI WAKE AUMBUKA, BOSI AANIKA UKWELI ALITAPELIWA

Leave A Reply