The House of Favourite Newspapers

Lavaud Agonga Kolabo ya Kibabe na Tiwa Savage, Reekado Banks, Patoraking Kwenye Roll On Me

0

STAA wa kike kwenye uwezo mkubwa katika kuimba na kutunga, Lavaud amerejea kwa kishindo baada ya kuachia singo kali inayokwenda kwa jina la “Roll on Me” – ikiwa kwenye mitandao ya Saint & Citizen Music.

Katika singo hiyo, amewashirikisha mastaa kadhaa wa muziki Afrika wakiwemo, Tiwa Savage,
Patoranking, Reekado Banks na Kanis.

Kwa hakika mastaa hao wamezidi kuinogesha singo hiyo na kuifanya yenye ladha ya kipekee.

Kwenye “Roll on Me” kuna mikono ya maprodyuza wakali, kama Kel-P, ambaye amepata kufanya kazi na wasanii Burna Boy, Wizkid, Rema na Trakmatik.

Akizungumzia traki hiyo,
Lavaud anasema: “Nimefurahi sana kufanya kazi na wasanii wakubwa wenye uwezo na vipaji vya aina yake, lakini zaidi timu nzima ya utayarishaji. Nimependa jinsi tulivyoonyesha tamaduni na mila zetu za Kiafrika kwenye wimbo huo ambazo kwa hakika zimeongeza uzuri na upekee wa singo hiyo.”

Naye Tiwa Savage amesema: “Pale wasanii wanapokutana pamoja, kama hivi, kitu fulani cha kuvutia hutokea… na ndivyo ilivyokuwa.

“Huu wimbo ni mzuri na wa kipekee, nimefurahishwa na mchango wa kila mmoja wetu katika hii kazi.”

 

Leave A Reply