The House of Favourite Newspapers

Mwan­amama Ma­riah Carey Apandishwa Kizimbani Adaiwa Kuiba Wimbo wa Andy Stone

0
Staa wa wa muziki kutoka Marekani, mwan­amama Ma­riah Carey.

 

STAA wa wa muziki kutoka Marekani, mwan­amama Ma­riah Carey ameri­potiwa ku­fik­ishwa mahakam­ani kwa kosa la hatimiliki kupitia wimbo wake All I want for Christ­mas is You baada ya muimbaji mwingine Andy Stone kudai kuwa aliandika wimbo huo mwaka 1989.

 

Kwa mujibu wa nyaraka zilizodakwa na TMZ, Andy anadai kuwa wimbo huo ulipata ma­fanikio makubwa kwa kuingia kwenye charts za billboard 1993, huku wimbo wa Mariah Carey ulitoka 1994 ukiwa una­patikana kwenye album yake iliyoitwa Merry Christmas.

 

Andy Stone anasema kuwa Mariah na timu yake hawakuwahi kuomba kibali cha kutumia jina la wimbo huo hivyo anataka alipwe kiasi cha dola milioni 20 za Marekani ambazo ni takribani bilioni 46.5 za Tanzania.

Mpaka sasa hakuna ripoti yoyote kutoka kwa Mariah na timu yake juu ya madai hayo. Huku TMZ wakisema, Mariah akiwa na timu yake alionekana kwenye Mahakama Kuu ya Mji wa New Orleans.

GSM YAUNASA MKATABA WA STRAIKA MZAMBIA, SAIDOO ASIMULIA MAZITO | KROSI DONGO

Leave A Reply