The House of Favourite Newspapers

MWANAMKE MBARONI KWA KUMPIGA, KUMUUA MWANAYE

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana.
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanamke Rahel Matalaka, 41, mkazi wa kijiji cha Lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye Maliatabu Constantine, 10, mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Ikelege.
Tukio hil lilitokea tarehe 03.11.2018 majira ya saa moja usiku baada ya mama wa marehemu kuletewa malalamiko kuwa mtoto wake alikuwa akiangua na kuiba maembe kwa jirani ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadaye kufariki dunia.
Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga ili ionekane kuwa amejinyonga.   Majirani walipoona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao baada ya  kupata taarifa hizo walikwenda eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa.
Upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa  mahakamani na mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa  ndugu kwa ajili ya mazishi.
Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limekamata gari moja lililoibiwa lenye namba T.233 CDG aina ya Toyota Carina mali ya Renatus Elius mkazi wa mtaa wa Ghana, likiwa limetelekezwa kando ya barabara maeneo ya Kitangiri Wilayani Ilemela.
Gari hilo liliibiwa tarehe 01.11.2018, ambapo mmiliki wa gari alitoa taarifa polisi na baada ya  msako tarehe 04.11.2018 majira ya mchana gari lilipatikana  na wezi wakiwa wametoroka.
Ukaguzi wa gari hilo  uligundua baadhi ya vifaa vya gari hilo kutokuwepo, ambavyo ni betri, tairi moja, jeki, redio, power window na show ya mbele ya gari.
Polisi wanaendelea na msako kuwanasa wahusika wa wizi huo.
Wakati huohuo, Polisi mkoani Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye MALAGALITA MATHIAS, miaka 55, mkazi wa kijiji cha Nyatukala, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita 20 na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo moja, huko maene ya kijiji cha Nyatukala Wilayani Sengerema.
Tukio hilo limetokea tarehe 05/11/2018 majira ya saa 11 jioni. Hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa kwamba katika Vijiji vya Nyamizeze na Nyatukala vilivyopo Wilayani Sengerema wapo watu wanaojihusisha na uuzaji pamoja na utengenezaji wa pombe ya gongo na dawa za kulevya aina ya mirungi.
Aidha baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Polisi tulifanya msako mkali katika vijiji hivyo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi na mirungi huku wenzake wakifanikiwa kutoroka. Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini wenzake anaoshirikiana nao katika biashara hiyo haramu ya gongo na mirungu, pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Katika tukio la nne, mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku mbili hadi tatu ameokotwa akiwa hai baada ya kutupwa kichakani na mtu asiyefahamika kando ya Ziwa Victoria maeneo ya Bwiru wilayani Ilemela.
Tukio hilo limetokea tarehe 01.11.2018 majira ya nane mchana baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani, walipofuatilia walimkuta akiwa ameviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.
Mtoto amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri  ambapo amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru wilayani  Ilemela kwa ajili ya hifadhi. Polisi wanaendelea na upelelezi ambapo msako wa kumtafuta mama wa mtoto huyo unaendelea.
Katika tukio jingine, polisi mkoani humo, wanamshikilia mtu anayetuhumiwa kuwa tapeli/mwizi anayefahamika kwa jina la Benedicto Bahati, 29, mkazi wa Kiloleli, kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Tukio hilo limetokea tarehe 02.11.2018, majira ya saa 10 jioni baada ya mtuhumiwa kwenda kwa mtumishi wa benki ya CRDB tawi la Nyegezi -Malimbe na kudai yeye ni afisa wa TCRA Mkoa wa Mwanza, akisema alikuwa na taarifa zake ambazo zinaonesha alikuwa akifanya mawasiliano yasiyo rasmi.
Akaongeza kwamba alitumwa na ofisi ya TCRA Mwanza kufuatilia taarifa hizo, na kumtaka atoe fedha kiasi cha laki tano ili kumfichia siri hiyo kwa TCRA.
Baada ya hapo mlalamikaji alitoa taarifa polisi waliofanikiwa kumtia tapeli huyo nguvuni na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Katika tukio la sita, Polisi mkoa huo wamefanikiwa kukamata gari moja aina ya IST rangi ya Silver lenye namba T.892 DFY/DKY na pikipiki mbili,   moja yenye namba MC.836 ASK aina ya Boxer na nyingine aina ya Fekon isiyokuwa na namba. Gari na pikipiki hizo zimekamatwa baada ya kutumika katika matukio ya uhalifu  maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mwanza.
Polisi mkoani humo  imetoa onyo kwa wakazi wake waache vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, pindi mtoto wanapokosea waonywe ili kutambua makosa yao na si kuwapiga.  Pia vijana wamaonywa kuacha uhalifu ambao utawagharimuu maishani.

UNYAMA: Mama Amuua Mwanae Kisa Embe Dodo!!!

Comments are closed.