The House of Favourite Newspapers

Mwanamke kutoka Rwanda Afikisha Miaka 26 Akiwa na Maambukizi ya Ukimwi

0
Mwanamke kutoka Rwanda, Muneza Sylivie

Mwanamke kutoka Rwanda, Muneza Sylivie mwanzilishi wa shirika la RRP+ la wenye virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, amefahamisha kuwa amemaliza miaka 26 akiwa na ugonjwa wa Ukimwi.

Kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ilipelekea familia na hata majirani kumtenga baada ya kugundulika kuwa na maambukizi tangu mwaka wa 1998.

Amefahamisha kuwa ilifikia kubaki na kilo 12 katika mwili wake baada ya kutengwa na familia ambapo alikuja kupata ahueni baada ya kupata dawa za kufubaza virusi na baadae kuanzisha Shirika lake la kuwasaidia waathirika.

Hadi kufikia sasa shirika la RPP+ ina mashirika mengine 500 nchi nzima ambayo yamekuwa yakishirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi na kutoa mafunzo mbali mbali kwa wananchi.

MRITHI wa ZITTO KABWE DOROTHY SEMU AKITANGAZA MABADILIKO MAKUBWA NDANI ya ACT na UCHAGUZI…

Leave A Reply