The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Mkongwe Zaidi Duniani Afariki

0
Violet Mos Brown, enzi za uhai wake.
MWANAMKE mmoja wa Jamaica anayedhaniwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani, Violet Mos Brown amefariki akiwa na umri wa miaka 117  na siku 188.

Waziri Mkuu wa Jamaica alitangaza kufariki kwa mwanamke huyo kupitia mtandao wa Twitter. Vyombo vya habari vya nchini humo vilisema alifariki kwa utulivu katika hospitali moja katika mji wa Montego Bay.
Violet Moss Brown, aliyekuwa miongoni mwa wanawake watano wakongwe zaidi mapema mwaka huu, alizaliwa March 10, 1900. Alisema kuwa aliweza kuishi muda mrefu na kwamba aliweza kula karibu kila kitu isipokuwa nguruwe na kuku, pia hakunywa pombe kali.

Leave A Reply