The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Nyumba ya Zitto Kabwe Yateketea kwa Moto

0
Muonekano wa nyumba hiyo ikiendelea kuteketea kwa moto.
Moto ukiendelea kuwaka.

 

NYUMBA ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma yateketea kwa moto. Habari zaidi kuwajia baadae.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa, nyumba hiyo aliijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza na ipo Kibingo, Kata ya Mwandiga, Mjini Kigoma.

Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.

Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua na ilikuwa ikitumika kwa dharura.

Kwa upande wake, Mohammed Babu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ACT Amani (Ulinzi na Usalama) amesema wao kama chama wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko, na bado wanaendelea na kufuatilia, taarifa zikikamilika watawajulisha wananchi.

VIDEO

Leave A Reply