The House of Favourite Newspapers

Mwanamuziki Maarufu Morocco Akabiliwa na Kesi ya Ubakaji Nchini Ufaransa

0
Mwanamuziki nyota wa Morocco Saad Lamjarred

Mwanamuziki nyota wa Morocco Saad Lamjarred, anatuhumiwa na kesi ya ubakaji na unyanyasaji, ambayo imeanza kusikilizwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Mwanamuziki huyo maarufu anayeimba muziki wa pop wa Kiarabu, Bw Lamjarred anadaiwa kumbaka mwanamke mmoja wa Ufaransa katika hoteli ya kifahari huko Champs-Elysees mwaka wa 2016.

Lakini anakanusha madai hayo.

Video moja ya muziki za Bw Lamjarred imetazamwa na zaidi ya bilioni moja kwenye chaneli yake ya YouTube.

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco alimtunuku heshima ya juu zaidi ya kitaifa mwaka 2015.

Kama atakutwa na hatia, Bw Lamjarred anaweza kufungwa jela miaka 20.

Hukumu inatarajiwa kutoka siku ya Ijumaa.

SIMBA vs AZAM, MNYAMA KUSHUSHA MACHUNGU KWA AZAM? KOCHA ROBERTINHO AFUNGUKA…

Leave A Reply