The House of Favourite Newspapers

Mwanasiasa Kenya Akamatwa kwa Maadai ya Mauaji ya Mwanafunzi

Image result for Gavana Okoth Obado
Gavana Okoth Obado

Polisi nchini Kenya imemkamata Gavana Okoth Obado wa Jimbo la Migori Magharibi mwa nchi hiyo. 

Obado ataaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu, Sharon Otieno ukiendelea. Maafisa kutoka kitengo cha upelelezi wa uhalifu wa jinai, DCI wamemhoji kwa saa kadhaa leo.

Sharon
Marehemu Sharon Otieno Enzi za Uhai wake

Obado amekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye inasadikiwa alikuwa mpenzi wake. Polisi inasema Gavana huyo wa jimbo la Migori magharibi mwa Kenya atafikishwa mahakamani mjini Nairobi siku ya Jumatatu.

 

Wiki iliyopita, Obado aliwaambia polisi mjini Kisumu kwamba yeye binafsi angelipenda kuwajua wauaji wa Sharon ni kina nani. Wakili wake Obado, Cliff Ombeta anasema mteja wake hana hatia na kwamba amewaeleza polisi kila kitu alichofahamu kuhusiana na kesi hiyo.

 

Mwili wa Sharon ulipatikana ukiwa umetupwa kichakani eneo la Oyugis, Homa Bay mnamo 5 Septemba.Mtaalamu mkuu wa upasuaji wa maiti Kenya Johansen Oduor, baada ya kuuchunguza mwili wa marehemu, alisema mwanamke huyo huenda alifariki kutokana na kuvuja damu sana.

 

Alikuwa amedungwa kisu mara nane. Mwili huo pia ulikuwa na alama za kukabwa shingoni, na alama nyingine zinazoashiria kwamba alijaribu kujiokoa. Dkt Oduor alisema kuna uwezekano kwamba Sharon alibakwaSharon

Sharon anadaiwa kukutanishwa na mwandishi Barrack Oduor na diwani wa zamani wa eneo la Kanyidoto, Homa Bay Lawrence Mula ambaye alimfahamisha kwamba alikuwa na rafiki yake aliyetaka usaidizi wake kama mwanahabari.

 

Ni siku hiyo ambapo Sharon alikutana mara ya kwanza na Oduor ambapo alimwambia kwamba Gavana wa Migori Okoth Obado alikuwa amemtelekeza baada yake kubeba mimba yake. Familia yake imesitisha kwa muda usiojulikana mipango ya mazishi ya marehemu na Jumatano waliwaambia wanahabari kwamba wanasubiri matokeo ya uchunguzi kuhusu kifo chake.

Comments are closed.