The House of Favourite Newspapers

Mwanza: Maajabu ya Mti Kupiga Kelele Ukipinga Kung’olewa (VIDEO)

0

AMA kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! Taarifa zilizosambaa mitandaoni zimeeleza kuwa wakazi na watumiaji wa barabara ya Pasiansi Jijini Mwanza, jana jioni walipigwa butwaa baada ya kushuhudia kimbwanga ajabu cha mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using’olewe.

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.

Katika eneo la Pasiansi Jijini Mwanza mradi wa upanuzi wa barabara inayoelekea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaendelea.

Shughuli ya kuung’oa mti huo aina ya mwembe bado inaendelea leo ambapo inadaiwa mamia ya wananchi wamejitokeza kushuhudia tukio hilo.

================

Update

Taarifa ya kuwapo kwa mti uliodaiwa kulia machozi ya damu wakati ukikatwa zimekanushwa na Meneja wa TANROADS mkoani Mwanza.

Meneja huyo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Marwa Rubirya amesema habari za mti huo si za kweli na kuwa mti huo umeshakatwa.

“Huu ulikuwa uzushi hakuna kitu kama hicho sema kilichotokea ni kwamba mashine iliyopelekwa awali ilikuwa haina nguvu ikilinganishwa na ugumu wa mti huo,”amesema Rubirya.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kuzusha mambo ambayo hayana ukweli na kuibua hisia zisizo na msingi wowote.

Mwanza: Maajabu ya Mti Kupiga Kelele Ukipinga Kung’olewa

Leave A Reply