The House of Favourite Newspapers

Mwanza: Mtoto Aibiwa, Mama Yake Adanganyiwa Tsh. 10,000 Ya Kununua Mkate

0

Mtoto mwenye umri wa miezi minne ameibiwa katika mtaa wa ustawi wa jamii kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela jijini Mwanza.

 

Imeelezwa kuwa watu waliomuiba mtoto huyo wamemchukua mama mzazi wa mtoto huyo kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani lakini baada ya kufika Nyamanoro walimpa shilingi elfu kumi kwenda kununua mkate na baada ya kurudi amekuta tayari wameshaondoka na mtoto wake.

 

Wakizungumza kuhusu tukio hilo baadhi ya wananchi wamesema kuwa jambo hilo limewashangaza kwani wameshindwa kuelewa lengo la watu hao kumuiba mtoto huyo ni nini na kuwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao.

 

Akizungumza tukio hilo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi, amesema kuwa watu waliofanya tukio hilo mama mzazi wa mtoto anawafahamu hivyo jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao.

 

Hata hivyo Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kumuiba mtoto huyo na kwamba watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya dola.

 

Chanzo: MO dewjiblog

 

Live: Hatimaye Yanga Yafungukia Usajili wa Klabu Yake

Leave A Reply