The House of Favourite Newspapers

Mvua Yaua Watu Tisa Sengerema Mwanza

WATU tisa wa familia mbili, wakiwa ni wanawake wanne  na watoto watano, wamefariki katika Kata  ya Nyatukala wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, baada ya nyumba zao kukumbwa na maji kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya asubuhi, ilisababisha maafa hayo kwa baadhi ya nyumba ambazo zipo pembezoni mwa mto ambapo pia daraja muhimu limekatika na kukwamisha mawasiliano na usafiri katika maeneo hayo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Emmanuel Kipole, amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuondoka na kwenda katika maeneo ya muda ambayo tayari serikali imeyabainisha ili kuepusha madhara zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanz,a John Mongella,  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kuepusha kupoteza maisha ya wananchi wengine zaidi..

Miili yote  imepatikana na imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema, baada ya zoezi la uokoaji kufanywa na wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia nyavu na kamba.

Comments are closed.