MWENYE NYUMBA HAKAI FOLENI

HALOOOO eeehhh…vijana wa leo wanakwambia ukitaka kuona raha ya pombe povu lake na mjini hakuna mtoto mdogo ati ukikaa baa, basi we mtu mzima tayari hee heeeeiyaaaa! Shoga hakuna kitu kinachonikera kama mtu kujifanya mlango wa choo kupiga hodi huku unasikilizia utajibiwa nini!

 

Jamani mnazi tangu lini ukapandwa na mabuti ya mvua? Ona sasa hadi nimesahau kuwasalimia maana si kwa kushikwa koo huku najifanya natoa mihayo ya njaa kumbe moyoni ni uchovu tu, inahu? Shoga leo nimekereka, yaani ndiyo maana nakwambia limeniganda kama maji ya friza ukikatika tu umeme nayeyuka! Hivi kila siku nimekuwa wa kuwapa somo wanawake wenzangu, lakini mnashindwa kubadilika!

 

Nikisema huwa namaanisha shoga, unashangaa unaachwa kumbe wee ndiyo chanzo cha kuachwa! Mwanamke unajua usafi wa kuvaa wa mwili walaaa! Shuuuuutuuuu! Nimetumiwa meseji na msomaji wangu ambaye ameachwa, kisa uchafu na kunuka si kwapa hadi chumbani kwa bibi! Baada ya kunielezea, nikagundua kuwa kumbe kuachwa kwake alikutengeneza mwenyewe.

Anasema kuwa hadi sasa ameishi na wanaume watatu ndani ya mwaka mmoja na wote wamemuacha katika mazingira ambayo haamini. Nilipotaka kujua ni mazingira gani hayo ndipo akafunguka sasa! Acha autandike mkeka miye nikakaa namsikiliza, si unajua anti Naa tena!

 

Anasema kama ni kazi anayo tena mshahara si haba! Pesa hadi ya kuhonga mwanaume haimsumbui na ukija kwenye usafiri, achana na magari ya nyumbani kwao, anamiliki gari mbili za kifahari.

 

Nyumba amepanga kuuubwa ina kila kitu ndani hadi na hausigeli anayeongea Kingereza! Tatizo lake ni harufu tu bibiye ndiyo imemfanya akose wanaume. Anasema hata ajifanyie usafi mara ngapi atanuka tu, si nguo hadi chumba kizima hadi inafikia hatua anajiogopa.

 

Harufu hiyo imehamia sasa hadi kwenye magari yake na hata chumba chake cha ofisi japokuwa anajitahidi kuwasha AC na kupulizia viyoyozi juu, lakini ndiyo kwanza kama anamuogesha mtoto maji ya baridi akidhani hawezi kupiga kelele.

 

Shoga nikugeukie na wewe mwenye hali hii maana kuna wengine ni magonjwa na wengine kuendekeza kutojiweka safi. Mwanamke unatakiwa uwe safi kuanzia juu hadi chini, ndani kwako uwe msafi hata hiyo harufu mbona itakukimbia. Tatizo la msomaji huyu nilipombana aliniambia hata kusafisha kiwanja chake huwa mara mojamoja sana si kiwanja cha kwapani hadi kule kwa bibi! Ngachoka miyeee!

Hatukatai mwenye nyumba hakai foleni, lakini wakati mwin- gine ndiyo chanzo cha foleni kuwa naa mgogoro. Badilika mwanamke mwenzangu, siku hizi kuna manukato ya kila aina, safisha viwanja vyako kisha tumia manukato yako uone mwanaume gani atakukimbia? Kwa leo niishie hapa shoga, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine tamu.

 

Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu! Shoga nikugeukie na wewe mwenye hali hii maana kuna wengine ni magonjwa na wengine kuendekeza kutojiweka safi. Mwanamke unatakiwa uwe safi kuanzia juu hadi chini, ndani kwako uwe msafi hata hiyo harufu mbona itakukimbia…

 


Loading...

Toa comment