The House of Favourite Newspapers

Wakurugenzi Waswekwa Ndani kwa Kutoa Zawadi Hewa Mei Mosi – Video

MKUU wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey ameliagiza Jeshi la Polisi kuwaweka chini ya ulinzi Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Bukoba, Josephat Kyebyera na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Bukoba, Siima Kyamani kwa kutoa zawadi hewa kwa wafanyakazi bora katika halmashauri zao.

Mheluka aliyekuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera katika maadhimisho ya herehe za wafanyakazi (Mei Mosi), Mkoani humo, alimhoji Kyebyera iwapo amewapa zawadi wafanyakazi bora wa Halmashauri ya Bukoba aliokuwa amewaainisha.

Katika kujibu swali hilo, Kyebyera alisema zawadi zao za fedha tayari wameshawekewa kwenye akaunti zao za benki kama ilivyotakiwa na Serikali.

Lakini walipoitwa wafanyakazi hao na kuulizwa iwapo kuna yeyote amewekewa fedha zake kwenye akaunti yake, wote walikataa na kusema hawajaingiziwa fedha hata shilingi moja.

Hivyo ikatoka amri ya kukamatwa mara moja kwa ofisa huyo kwa udanganyifu alioufanya.

VIDO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.