The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti wa Wazazi CCM Morogoro Ahimiza Umoja, Atoa Kadi 500 Kila Wilaya

0
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk Rose Rwakatare, amehitimisha ziara yake mkoani humo akiwataka viongozi kuhakikisha wanaanzisha miradi ya kiuchumi ya Jumuiya.
Dk. Rose amesema kila Wilaya ihakikishe inakuwa na nyumba za watumishi wa Jumuiya hiyo na kusisitiza umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya hiyo.
Akizungumza wakati akihitimisha ziara hiyo Morogoro Mjini, Dk. Rose aliwaasa wazazi kusimamia maadili mema katika jamii na kupinga vitendo vya  ukatili wa  kijinsia na matumizi ya dawa za kulevya.
Alitembelea  watu wenye mahitaji maalum kuwafariji kwa kuwapa baadhi ya mahitaji mbalimbali na kuiasa jamii kujenga utamaduni wa kutembelea familia zenye mahitaji ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali .
Dk. Rose alisisitiza  uhai wa chama  na  Jumuiya ya Wazazi  na alikagua miradi mbalimbali  ya Jumuiya na serikali huku akisisitiza viongozi kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto zinaikabili Jumuiya hiyo .
Mwenyekiti huyo pia alikagua miradi  ya ufugaji wa kuku na ujenzi wa nyumba ya  mtumishi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Gairo na  Wilaya kilombero na kuahidi kuwa atasaidia ujenzi wa nyumba hizo.
k. Rose pian aliahidi  kuchangia mifuko ya saruji katika ujenzi wa Zahati ya Ipopoo na kuwapatia taulo za kike  wanafunzi wa ya sekondari Miembeni  Wilaya ya Malinyi.
Katika ziara hiyo, Dk Rose alikagua mradi wa shamba la mikorosho na kuchangia  pesa kwaajili yakununua kiwanja  cha ujenzi wa nyumba  ya mtumishi wa CCM  Wilaya ya Morogoro Mjini na kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kufugia samaki.
Kutokana  na changamoto ya usajili wa wanachama wapya  wa Jumiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose aliwakakadhi  kadi 500  za  Jumuiya  ya Wazazi kwa kila Wilaya na kuwaelekeza viongozi wa Jumuiya  wa  Wilaya hizo kuhakisha wanaongeza  idadi ya wanachama wasiopungua  100 kwa mwezi.
Dk  Rose alihamasisha umuhimu wa michezo  kwa kutoa vifaa ya michezo  wilaya zote alizotembelea ikiwemo jezi  na mipira ya miguu ili wawezekuanzisha ligi katika wilaya zao na kutumia fursa hiyo kupata wanachama wapya wa jumuiya ya wazazi.
Leave A Reply