The House of Favourite Newspapers

MWIJAGE  AWATAKA WAFANYABIASHARA KUZALISHA BIDHAA ZENYE TIJA

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (katikati) akipata maelezo kwa mmoja wa wafanyabiashara katika Maonyosho ya Bidhaa Sabasaba Viwanja vya Mwalimu Nyerere katika  barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mwijage (katikati) akizungumza na  mmoja wa wafanyabiashara katika Maonyosho ya Bidhaa Sabasaba.
Wafanyabiashara mbalimbali wakiendelea kumweleza jambo Mwijage juu ya bidhaa zao wanazozitangaza kwenye maonyesho hayo.

WAZIRI wa viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wafanyabiashara nchini kuzalisha kwa viwango na tija kulingana na viwango vya kimataifa.

 

Akizungumza  mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mabanda ya Maonyesho  42 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) yanayofanyika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade) ambapo watakutana wajasiliamali na wazalishaji wakubwa kutoka ndani na nje ya nchi, Mwijage amesema kama wafanyabiashara wa Tanzania watashindwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali katika kuboresha biashara zao ni wazi kwamba nchi itakua imepoteza fursa adhimu kibiashara.

 

Amesema mbali na maonyesho hayo serikali itatoa matrekta elfu 2400 kwa wakulima wakubwa na wakati ambayo yatakwenda shambani kwaajili ya kukuza kilimo cha kisasa na kuzalisha kwa tija ili viwanda vipate malighafi za kutengeneza bidhaa kwa

 

Maonyesho ya 47 ya Sabasaba yanatarajiwa kufunguliwa na waziri Mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli Jumatatu ya Jualai 2, 2018.Zaidi ya  makampuni 500 na nchi zaidi ya 20 zimejiandikisha kushiriki maonyesho hayo.

Comments are closed.