The House of Favourite Newspapers

Muroto; Muasisi wa Msemo ‘Watapata Tabu Sana’ Mnayenyoosha Masela!

HIVI karibuni nikiwa naangalia mashindano ya Kombe la Dunia kati ya Ureno na Iran, shabiki mmoja wa Timu ya Ureno wakati timu yake inaingia uwanjani alisi­mama na kusema; ‘hawa Iran watapata tabu sana… kipigo watakachokipata ni cha mbwa koko’.

 

Basi unaambiwa baada ya kijana huyo kutamka maneno hayo, uku­mbi ulilipuka kwa vicheko. Wengi wakaanza kujadili maneno hayo. Kijana huyo hakuwa wa kwanza kuyatamka bali huko mtaani msemo huo umekuwa maarufu sana.

Kwenye mitandao ya kijamii wengi wamekuwa wakiutumia ka­tika mazingira tofauti lakini naamini wapo ambao mpaka leo hawamjui mwasisi wake.

 

 

Huyu si mwingine, ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto. Kamanda huyu amekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni ukiacha yule Kamanda wa Polisi wa Pemba, Has­san Nassir ‘Kamanda wa Kukohoa’, ambaye alieleza kuwa, mwanaume yeyote atakayekohoa baada ya kuona mwanamke ‘aliyefungashia’, Jeshi la Polisi litamshughulikia.

 

Huyo naye alitrend sana kwenye mitandao na vyombo mbalimbali vya habari. Lakini kwa sasa Ka­manda Muroto amekuwa kwenye midomo ya wengi.

Kabla ya kuwakumbushia ilikuwaje mpaka akatamka maneno hayo, niseme tu kwamba nimemjua vizuri kamanda huyu tangu alipokuwa Kamanda wa Polisi Temeke jijini Dar.

 

Kipindi hicho miaka ya 2016/17 amekuwa mwiba kwa wahalifu wa eneo lake na wachambuzi wa masuala ya usalama watakubal­iana nami kwamba, enzi zake pale Temeke alikuwa akisumbua na hata matukio ya kihalifu yalipun­gua kwa kiasi kikubwa.

 

Staili yake ya kuwanyoosha ‘masela’ hasa wale waliokuwa wakikamatwa na bangi, uzururaji pamoja na matukio ya panya road enzi zile, ilikuwa ya kipekee na iliyozaa matunda. Alichokuwa akifanya, ukikamatwa kwenye tukio la kihalifu, waandi­shi wanaitwa, wahalifu wote wanapangwa mstari kila mmoja anata­jiwa kosa lake kisha anaulizwa; ‘kwa nini umefanya kosa hili? Utafanya tena? Unadhani bangi inakusaidia chochote? Na maswali mengine kama hayo.

 

Achana na hao wahalifu wadogowadogo, matukio ya ujambazi nayo enzi zake yali­pungua kwa kiwango kikubwa, itoshe tu kusema kwamba, kamanda huyu ni mchapa­kazi na yawezekana ndiyo maana akahamishiwa Do­doma ambako nako anapiga mzigo si wa kitoto hadi mdau mmoja aliwahi kusema Muroto ni mwiba kwa wahalifu. Wavuta bangi, majambazi na wahalifu wengine mkoani Dodoma sasa ‘wamekaa’.

Akiwa Dodoma, mara kadhaa amekuwa akionekana kwenye vyombo vya habari akiwanadi wahalifu mbalimbali na staili yake ile aliyotoka nayo Temeke imeendelea kuwa kivutio. Uta­kumbuka kipindi kile alipokamat­wa Nabii Tito (picha kubwa juu), yule aliyekuwa akijidai Mtumishi wa Mungu lakini kumbe alikuwa feki.

Pia utakumbuka siku ambayo msanii wa muziki Bongo, Rashidi Makwilo ‘Chid Benz’ alinaswa na bangi. Jinsi alivyomnadi staa huyo ilikuwa ya kipekee sana, video zake zikasambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini, kipindi kile ambacho taifa lilikuwa likikabiliwa na tishio la watu kuandamana, wakati akiongea na waandishi wa habari, Kamanda Muroto alisema: “Wanaofikiria kuandamana watapata tabu sana….nasema watapata tabu sana. Kipigo chake kitakuwa ni cha mbwa koko.’

Maneno hayo yalimaanisha kwamba, watu am­bao wangekwenda kinyume na sheria wakaandamana, Jeshi la Polisi lingewafungia kazi. Kuan­zia hapo msemo huo umekuwa maarufu sana huko mtaani.

Gilles Muroto ni nani?

Ni kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma. Ni ofisa wa polisi aliyepitia ngazi mbalimbali za uongozi katika jeshi hilo.

Kabla hajafikia ngazi hiyo amepitia nafasi mbalimbali kama vile kuwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Arusha akifanya kazi chini ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha enzi hizo, Lebaratus Sabas.

Akiwa Arusha, Kamanda Muroto alikorofishana sana na wanasiasa wa upinzani hasa Mbunge wa Arusha Mjini, Godb­less Lema kwani siku moja ali­wahi kumzuia kufanya mikutano ya kisiasa wilayani hapo.

Kamanda Muroto alipandish­wa cheo na kuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke ambako alifanya kazi kubwa ya kuzuia uhalifu na kubwa ni kulidhibiti kundi la ‘panya rodi’, ambalo lilikuwa tishio katika eneo lake la Temeke kama Mkoa wa Kipolisi.

Katika mabadiliko aliyofanya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, (IGP) Simon Sirro, Kamanda Muroto alihamishiwa mkoani Dodoma ambako amekuwa ka­manda wa polisi (RPC) mkoani humo hadi tunapoandika makala haya.

 

”Sio Kwa Kipigo Cha Mbwa Koko Bali Ni Utulivu Wao” -Kamanda Muroto

Comments are closed.