The House of Favourite Newspapers

MWIJAGE AZINDUA KITUO CHA USAMBAZAJI VIFAA VYA UJENZI

0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha usambazaji wa vifaa vya ujenzi huko Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambako alikizindua kwa kuweka jiwe la msingi leo.
. …Akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.
Balozi wa China nchini, Bi Wang Ke, akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni na wadau waliohudhuria tukio hilo.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, akizungumza katika hafla hiyo.
Uzinduzi wa kituo hicho ukifanyika.
Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria tukio hilo.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, leo ameweka jiwe la msingi katika kituo cha usambazaji  eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.

 

Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

 

Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.

 

Alisisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.

 

Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu.

 

Leave A Reply