The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Agnes Almasy wa ITV Waagwa Dar – Video

0

MWILI wa aliyekuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa ITV, Agnes Almasy aliyefariki dunia gafla juzi umeagwa katika Kanisa la Anglikana, St. Nicholaus – Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Septemba 5, 2020.

 

Simanzi na majonzi vimetawala miongoni mwa wafanyakazi wenzake, ndugu, majirani na waombolezaji waliofika kanisani hapo kuungana na wanafamilia kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwiosho kwa mpendwa wao huyo.

 

 

Agnes alifariki ghafla dunia juzi Jumatano, Septemba 3, wakati akiwa njiani kuepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

 

 

Mwili wa Agnes unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Bombo Mkoani Tanga kesho baada ya kuagwa leo na kuanza safari ya kupelekwa nyumbani kwao Tanga.

 

Baadhi ya majirani walioishi karibu na marehemu Agnes wamesema alikuwa ni mtu mkarimu asiyekuwa na majivuno na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii.

 

Uongozi wa ITV/Radio One umesema umempoteza mfanyakazi aliyekuwa anapenda taaluma yake ya habari kwa kufanya kazi kwa kujituma katika utendaji wake wa kazi wakati wa uhai wake.

 

 

Agnes alihitimu Stashada katika Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam, ambapo baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Lovely Professional University kilichopo nchini India na kupata Shahada ya Uandishi wa Habari na Umma mwaka 2017. Aliajiriwa  katika kituo cha utangazaji cha ITV Machi 19, 2018, akiwa mwandishi wa habari. Marehemu Agnes ameacha mume na mtoto mmoja wa kike.

 

Leave A Reply