The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Bilionea Subhash Patel Ulivyoingizwa Makabuli ya Kijitonyama

0
Mwili ukiingizwa eneo la makabuli hayo.

ALIYEKUWA Mfanyabiashara Bilionea, Subhash Patel hivi ndiyo mwili wake ulivyowasili kwenye makabuli ya Wahindi ya Kijitonyama Jijini Dar na kupokelewa na waombolezaji kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mazishi kwenye makabuli.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambaye ametajwa kama rafiki mkubwa wa marehemu tangu walipokuwa watoto ndiye aliyeongoza taratibu za kuuhifadhi mwili huo kwenye makazi ya milele.

Angalia picha

Waombolezaji wakiwa na huzuni.

 

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akisalimina na mmoja wa waombolezaji baada ya kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu.

 

Mfadhili wa zamani wa Timu ya Simba SC Azim Dewj akiwa na huzuni eneo la tukio.

 

Baadhi ya wa makampuni yaliyoachwa na marehemu wakiangalia kwa mbali taratibu za mazishi ya aliyekuwa bosi wao.
Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete akizungumza na mmoja wa waombolezaji.

 

Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia kikaribu yaliyokuwa yakiendelea.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply