The House of Favourite Newspapers

Vilio, Simanzi Miili 12 Ikiagwa, Mmoja Ashindwa Kutambulika – Video

0

HAKIKA  ilikuwa ni simanzi pale familia ya Mzee Mkama Mayunga ilipopoteza jumla ya ndugu wanane ambao walikuwa wakiishi Mtaa wa Nyerere B Kata ya Mabatini wilayani Nyamagana jijini Mwanza, tukio ambalo limesabaaisha mama mzazi wa watoto hao wanane waliofariki, Asha Mkama,  kulazwa mpaka sasa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza,  Sekou Toure kutokana na kupoteza fahamu mara kwa mara sababu ya vifo  hivyo vya watoto wake tena wa kuwazaa mwenyewe.

Katika msiba huo ambao ulikuwa unaonekana wazi kuwa ni msiba wa taifa, ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanzam John Mongella, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula,  na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Philis Nyimbi pamoja na viongozi wengine wa kisiasa ambao kwa pamoja walifika Mabatini kuungana na ndugu jamaa waliopoteza ndugu zao katika ajali iliyotokea Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu 15 papo hapo.

Global Publishers imezungumza na msemaji wa familia Bi, Mwahija Mussa Msalika ambaye alisema kuwa: “Kiukweli familia yetu imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na ndugu wanane, ni majonzi ambayo hayaelezeki lakini hatuna budi kuyakubali kwa kuwa ndiyo kazi ya Mola.”

 

Aidha,  alisisistiza kuwa: “Miongoni mwa waliopata ajali na kufariki yupo binti ambaye  alikuwa rafiki yake na Rehema Hussein  amefariki dunia pia  yeye mpaka sasa hajatambulika na alikuwepo kwenye safari ya kwenda Singida katika harusi na mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Mwanza kwa hivyo nawaomba ndugu wa dada huyo wajitokeze kumchukua ndugu yao kwa ajili ya kumstiri.”

Hata hivyo Aisha alisema kwamba bwana harusi ambaye alikuwa anakwenda kufunga ndoa mkoani Singida bado mzima na amepelekwa hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Mhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi kwa kuwa amepata maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake, hali ambayo inawalazimu ndugu kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya kuunganishiwa mifupa ambayo imevunjika.

Waliofikishwa nyumbani  ni pamoja na Zakia Ibrahim, Lamlat Mkama, Swalaia Ibrahim akiwa na mtoto wake, Rehema Hussein, Angel George, Halima Rashid, Ustadh Mrisho pamoja na Majaliwa Paschal, hawa miili yao ilifikisha Mabatini kwa ajili ya kuombewa dua na baadaye ilikwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Mlango Mmoja huku Majaliwa Paschal akizikwa Maduka Tisa.

Habari/Picha na JOHNSON JAMES- GPL

 

Leave A Reply