The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Dk Massawe Waagwa Muhimbili – (Pichaz+Video)

0

MWILI wa aliyekuwa daktari bingwa wa magonjwa ya watoto, Dk. Augustine Massawe umewasili katika viunga vya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) kwa ajili ya kuagwa leo Jumatatu, Agosti 16, 2021.

Dk Massawe  Massawe alifariki dunia Ijumaa iliyopita, Agosti 13, 2021 wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) .

Dk Massawe alikuwa daktari maarufu ambaye amekuwa akitibu watoto tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980 na alipata umaarufu mkubwa katika jijini la Dar es Salaam kutokana na huduma ambayo aliyokuwa akiitoa.

Kutokana na kujituma kwake, licha ya kustaafu miaka 10 iliyopita Muhimbili ilimuomba aendelee kutoa huduma na hadi anafariki alikuwa bado akihudumia watoto hospitalini hapo na akiendelea kufundisha wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS).

Mtoto mkubwa wa marehemu DK Furaha Agosti amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upumuaji.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply