The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Dotto Mzava wa JF wasafirishwa kwenda Same kwa mazishi

0

1

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Jamii Forum, Dotto Mzava likishushwa kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Wasabato Manzese Uzuri jijini Dar kwa ajili ya sala ya kabla ya kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro leo.

2

Mchungaji wa Kanisa la Adventist Wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same, Kilimanjaro.

3

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Mello akitoa historia fupi ya marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.

4

Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa.

5

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya kusafirishwa kuelekea Same, Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho.

6

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa kuelekea Same mkoani Kilimanjaro mapema leo.

Picha na Richard Mwaikenda Blog

Leave A Reply