Joseph Senga enzi za uhai wake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016.
Dada wa Marehemu akilia kwa uchungu.
Jeneza lenye mwili wa likiingizwa kanisani kwa ajili ya maombezi.