The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Dr. Mengi Ulivyoagwa Karimjee Dar (Picha + Video)

Mke wa marehemu Mengi Jacqueline Ntuyabaliwe akiaga mwili wa Mengi leo Karimjee, jijini Dar.

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi, umeagwa leo Mei 7, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville (aliyekaa kwenye meza), akiaga mwili wa Mengi.

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu wameungana na familia ya marehemu na waombolezaji wote kuuga mwili huo.

Mtoto wa Mengi, Abdiel Mengi akiaga

Baada ya kuagwa utasafirishwa kesho kwenda kijijini kwao Machame mkoani Kilimanjaro ambako utazikwa siku ya Alhamisi.

Msanii wa bongo Movie, Steve Nyerere akiaga mwili.
James Mbatia (wa mbele) mbunge wa Vunjo katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
Mwili wa Marehemu ukiingizwa kwenye gari baada ya kuagwa viwanja vya Karimjee.
Wanahabari wakiwa kazini wakati mwili ukiondoka viwanja vya Karimjee.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.