The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mmiliki wa Super Sami Wawasili Nyumbani Kwake

Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake.

 

MWILI wa mfanyabiashara na mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Super Sami, Samson Josiah umewasili nyumbani kwake leo Ijumaa, Machi 16, 2018 Mtaa wa Majengo Mapya wilayani Magu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 

Mwili wa Samson uliokotwa juzi jioni baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser kukutwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara, Ijumaa iliyopita.

 

 

Samson enzi za uhai wake.

 

Kwa mujibu wa familia ya Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa kwake ambayo ni Februari 27, majira ya usiku, alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

 

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa na Kagera.

 

Jeshi la Polisi mkoani Mara limesema limewatia mbaroni watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara huyo.

Comments are closed.