The House of Favourite Newspapers

WOLPER; KIBOKO KWA KOPI & PASTE

Wolper kwenye Shoo na Papii Kocha.

HAKUNA kitu kizuri duniani kama kubarikiwa kuwa na kipaji ambacho unaweza kukifanya na jamii ikakukubali.

Jacqueline Wolper ni mmoja kati ya wasanii waliobarikiwa kuwa na vipaji, ukiachana na kuigiza ambapo ndipo kumem­patia jina, Wolper ni bonge la mbunifu wa mavazi.

 

 

Ameshawavalisha mastaa wengi na pia amekuwa akibuni mavazi yake mwenyewe yanayo­tambulika kama ‘parachuti’.

Kuiga si dhambi, lakini kwa siku za hivi karibuni mavazi mengi ambayo Wolper amekuwa akionekana nayo ama kuwabu­nia watu basi yanakuwa ni kopi na pesti kutoka kwa mastaa wa Marekani akiwemo staa wa Muziki wa Pop, Rihanna.

Katika makala haya yanach­ambua baadhi ya mavazi hayo;

Cardi B.

 

UZINDUZI WA NUMBER ONE

Katika uzinduzi wa video ya Wimbo wa Number One ya Diamond uliofanyika ndani ya Hoteli ya Serena, Wolper alito­kelezea na gauni ambalo wiki hiyohiyo Rihana alikuwa amelitinga katika Tuzo za Grammy.

 

UZINDUZI WA CHANELI

Mbali na kupenda kukopi mavazi hayo ya Rihanna na kutokelezea, ishu nyingine ilikuwa katika uzinduzi wa chaneli ya kiswahili ya filamu inayopatikanika ka­tika king’amuzi cha Dstv.

Katika usiku huo, Wolper alitokelezea na gauni kubwa jeusi la parachuti ambapo gauni kama hilo liliwahi kuvaliwa na Rihanna lakini utaofauti wake ukawa ni rangi kwani la Rihanna lilikuwa la ‘light blue’.

Rihanna.

BIRTHDAY YA SWEET FELLA

Hii nayo iliongelewa sana mitandaoni baada ya Wolper kumbunia gauni jeupe mke wa Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella aitwaye Sweet.

Sweet Fella alitinga gauni hilo siku yake ya kuzaliwa ambapo lilikuja kujulikana kuwa, Wolper alilipesti kutoka kwa Rihanna.

SHOO YA PAPII

Juzikati katika shoo ya kwanza kwa wanamuziki ndugu, Papii na Babu Seya iliyofanyika katika Ukumbi wa King Solomon, Wolper alitinga tena na gauni la kupesti.

Katika usiku huo, Wolper aliingia akiwa na parachuti la rangi ya ‘damu ya mzee’ ambalo ilibainika amelip­esti kutoka kwa rapa wa kike, Cardi B.

 

NA IMELDA MTEMA.

SPOTI XTRA LAANZA KUMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA BEATS BY DRE

Comments are closed.