The House of Favourite Newspapers

MWILI WA MSANII BONGO WAAGWA DAR

Jeneza lenye mwili wa marehemu Mgonahazeru likifikishwa nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar kwa ajili ya ibada ya heshima za mwisho na kisha kusafishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa mazishi.

MWILI wa aliyekuwa mwanamuziki wa Bendi ya Vijana Jazz, Abdallah Mgonahazeru umeagwa leo Ijumaa, nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao katika Kijiji cha Kinole mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko.

 

Mgonahazeru ambaye alijiunga na bendi 1983, alifariki juzi Alhamisi katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa maradhi ya henia ambapo kifo chake kimeacha simanzi kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

 

Akiswaliwa.

 

Watu mbalimbali wamefika kuungana na familia, ndugu na marafiki kwa ajili ya kuuaga mwili huo wakiwemo wasanii Max Bushoke, Mzee John Kitime, Shaka Zulu, Rehema Tajiri, wasanii wa Bongo Movies, Chopa Mchopanga, Simon Mwakifwamba na wengine.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un!

Comments are closed.