WANAHABARI nchini wameombwa kuendeleza amani na upendo katika kumuenzi marehemu, Mayage S. Mayage liyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam kama ishara ya kuiga matendo mema aliyoyatenda enzi za uhai wake.
Hayo yamesemwa leo na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada fupi ya mazishi ya kumuaga Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Akiendesha misa hiyo, Padre Kaniki alisema msiba ni sehemu ya kujifunza kutenda yaliyo mema kwa wale wanaobaki hivyo ni vyema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.
Kwa upande wa familia ikisoma risala ilisema kuwa wakati wa uhai wake marehemu alisoma katika vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi na baada ya kuhitimu alifanya kazi katika maeneo mbalimbali.
Naye Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Saleh Ally akizungumza kwa niaba ya kampuni amaemuelezea marehemu kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika tasnia ya habari kwani ni alitanguliza mbele maslahi ya kazi kuliko vitu vingine na hivyo akasema ni pigo kwa familia na jamii kwa ujumla
Comments are closed.