The House of Favourite Newspapers

Aliyekaa Mochwa Mochwari Miezi 8 Azikwa

0

Hatimaye Mwili wa Wilson Ogeta mkazi wa Nyambogo Wilayani Rorya uliokaa miezi 8 mochwari, umezikwa kwa usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka.

 

Wanafamilia wa marehemu wameiomba serikali kusimamia eneo la marehemu kurejeshwa kwa mjane ili kuendeleza shughuli za uzalishaji.

 

Mzee Ogeta alikuwa akiishi katika kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya Mkoani Mara , alifariki dunia akiwa na miaka 89 na familia yake kushindwa kumzika baba yao huyo mzazi baada ya kuibuka mgogoro mkubwa wa mirathi.

 

Leave A Reply