The House of Favourite Newspapers

Mwimbaji wa FM Academia, Malu Stonchi Aanguka Jukwaani na Kufariki Dunia

0

Mwimbaji nyota wa FM Academia, Malu Stonch amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla jukwaani.

Tukio hilo limetokea katika Ukumbi wa Target, Mbezi Beach, Jumamosi usiku wakati mwimbaji huyo akiwa jukwaani anaimba wimbo wa ‘Hadija’.

Inaelezwa kuwa wakati anaimba wimbo huyo, Malu Stonch alidondoka ghafla na kupoteza fahamu.

Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza huku akiwa bado hajitambui, ndipo akakimbizwa Masana Hospital.

Mwanahabari na mdau mkubwa wa muziki, MC Petit aliyekuwa miongoni mwa waliomkimbiza Malu Stonch hospital, amethibitisha taarifa za kifo cha mwimbaji huyo.

“Pale Masana walipompokea tu, wakatuambia tumpeleke Lugalo Hospital kwa kuwa mgonjwa wetu ameshafariki. Tulipofika Lugalo nao wakatuthibitishia kuwa Malu Stonch amefariki na hivyo tukafanya utaratibu wa kumpeleka chumba cha kuhifadhi maiti,” alisema MC Petit.

Taarifa zaidi zitakujia kupitia hapahapa.

Credit: Said Mdoe, Saluti5

Leave A Reply